Dodoma FM
Dodoma FM
14 October 2025, 2:33 pm

Picha ni baadhi ya mabondia watakaoshiriki katika pambano la ngumi Kibaigwa. Picha na Hamis Makila.
Pambano la ngumi Kibaigwa limeahirishwa hadi Oktoba 25 huku mabondia wakipimwa afya zao kabla ya kushiriki.
Na Hamis Makila.
Pambano la ngumi lililopangwa Kibaigwa limeahirishwa hadi Oktoba 25 baada ya kugundulika kuwa mabondia hawajapimwa afya zao kwa wakati, hatua inayolenga kuhakikisha usalama wa washiriki.
Mkurugenzi wa Kikundi cha Ngumi cha Wizard Fitness Dodoma, Yuko Kiyando, amesema kuwa pambano lililopangwa kufanyika Oktoba 18 katika Uwanja wa Amani, Kibaigwa limeahirishwa ili mabondia wote wapimwe afya zao kabla ya kushiriki.
Baadhi ya mabondia waliojihusisha na maandalizi ya pambano hilo wameeleza kuwa wanajiandaa kikamilifu ili kufanikisha ushindi.
Pambano litashirikisha mabondia 25 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania, huku pambano kuu ni kati ya Anthony Boika kutoka Dodoma na George Dimoso kutoka Dar es Salaam.