Dodoma FM

Changamoto ya maji Chanhumba karibu kutatuliwa

14 October 2025, 12:13 pm

Changamoto ya kukosekana kwa umeme iliwalazimu kununua maji kutoka maeneo ya mbali, jambo lililoongeza gharama za maji. Picha na Mtandao.

Hatua ya kufungwa kwa transifoma mpya katika kijiji cha Chanhumba italeta faraja kwa wananchi waliokuwa wakikabiliwa na upungufu wa maji.

Na Victor Chigwada.

Wananchi wa Kijiji cha Chanhumba, Kata ya Handali, Wilaya ya Chamwino, wameanza kupata matumaini juu ya utatuzi wa changamoto ya kukosekana kwa mashine ya maji sanjali na kufungiwa kwa transifoma mpya kisimani.

Baadhi ya wananchi wamesema kwamba changamoto ya kukosekana kwa umeme iliwalazimu kununua maji kutoka maeneo ya mbali, jambo lililoongeza gharama za maji.

Hata hivyo, kupitia ufumbuzi wa kuwekwa kwa transifoma mpya, watapata huduma ya maji bila mashaka yoyote.

Sauti za wananchi.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Chanhumba, Ndg. Amosi Lusiji, amesema changamoto iliyopo kisimani ni kukosekana kwa mashine ya kufua umeme wa kujitegemea, jambo ambalo limekuwa likipunguza nguvu ya kuvuta maji kutokana na matumizi ya wananchi.

Lusiji ameongeza kuwa tayari amewasiliana na watu wanaohusika na nishati ya umeme, na wameahidi kuwaletea mashine mpya ya kufua umeme ya kujitegemea kisimani.

Sauti ya Amosi Lusiji.

Aidha, amesema pamoja na kuwaletea mashine mpya, wamefanya utafiti na kugundua changamoto pia ipo kwenye mota ya maji, hivyo watashirikiana na fundi husika ili kubadilisha na kurekebisha ili huduma ya maji ipatikane kwa ufanisi.

Sauti ya Amosi Lusiji.