Dodoma FM
Dodoma FM
13 October 2025, 1:50 pm

Picha ni aliyekuwa Kocha Mkuu wa Dodoma jiji FC Vicent Mashami. Picha na ukurasa wa Dodoma Jiji FC
Kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara, kila timu inatakiwa kuwa na kocha mwenye leseni ya kiwango kinachokubalika na Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Na Hamis Makila.
Dodoma Jiji FC imechukua hatua ya kumsimamisha kocha mkuu na kumtumia kocha wa muda kuiongoza timu, baada ya kushindwa kutimiza vigezo vya kikanuni vya leseni, huku klabu ikiendelea kulipa faini kwa kukiuka kanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Afisa Habari na Mawasiliano wa Kikosi cha Dodoma Jiji FC, Moses Mpunga, amesema kikosi chao kimeshamtufata kocha wa muda atakayekiongoza kikosi hicho, kutokana na kocha mkuu, Vicent Mashami, kukosa vigezo vya kikanuni vya kulisimamia benchi la ufundi.
Kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara, kila timu inatakiwa kuwa na kocha mwenye leseni ya kiwango kinachokubalika na Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Hata hivyo, Dodoma Jiji ilionekana kukiuka kanuni hiyo katika michezo yake mitatu iliyopita dhidi ya KMC, TRA United, na Coastal Union. Kwa kila mchezo, klabu hiyo imepigwa faini ya sh. milioni 5, ikifanya jumla kufikia sh. milioni 15. Adhabu hiyo imetajwa kama onyo kwa klabu nyingine kuhakikisha zinazingatia matakwa ya kikanuni, hususan kuhusu makocha wenye leseni halali.
Akizungumza na Kipindi cha Michezo Bab Kubwa, Mpunga amesema kocha wa muda tayari amepatikana na atakuwepo kwenye benchi la ufundi la Dodoma Jiji katika mchezo dhidi ya Fountain Gate, utakaopigwa Oktoba 17 kwenye Dimba la Tanzania te Kwara, Babati, Manyara.