Dodoma FM
Dodoma FM
13 October 2025, 11:22 am

Picha ni Mwanasheria wa Baraza la Machifu Tanzania akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dodoma. Picha na Selemani Kodima.
Watanzania watakiwa kujihadhari na taarifa zisizo sahihi zinazotolewa kwenye mitandaoni ya kijamii zenye lengo la kupotosha umma kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 29.
Na Selemani Kodima.
Watanzania wameshauriwa kujihadhari na mitandao ya feki ya kijamii inayopotosha tunapoekelea kwenye uchaguzi kuu wa Urais, Wabunge na Madiwani ambayo imekuwa ikitoa taarifa zisizo sahihi na kuhatarisha kutoweka kwa amani na utulivu wa nchi.
Rai hiyo imetolewa na Mwanasheria wa Baraza la Machifu Tanzania alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Dodoma alipokuwa akiwasisitizia watanzania kujihadhari na taarifa zisizo sahihi zinazotolewa kwenye mitandaoni inayopotosha umma kuelekea kwenye kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi huo muhimu.
Amesema kuwa kuna watu wametengeneza mifumo feki kwenye mitandao ya kijamii ambayo imekuwa ikitoa taarifa za upotoshaji na zenye kutishia amani na utulivu na hasa kuelekea kwenye uchaguzi huo kwa madai kuwa hatafanyika.
Mwana sheria huyo pia amewataka vijana kujiepusha na wanasiasa ambao hutumia nafasi zao kutaka kuwapotosha kwa lengo la kuwahamamsisha uvujifu wa amani kutokana na vyama vyao vya siasa kutokuwa na sera wala ilani itakayoweza kuleta mabadiliko ya kiuchumi.

Naye Mwenyekiti wa Wanawake na Samia Mkoa wa Dodoma Fatuma Madidi amewaomba wakina mama kuhakikisha wanatoa elimu kwa wengine juu ya madhara yanayotokea pindi nchi inapokuwa na machafuko baada ya kukosa amani na utulivu.
Madidi ameongeza kuwa mara nyingi yanapotokea machafuko yoyote ndani ya nchi wahadhirika wakubwa ni watoto,wanawake na watu wenye ulemavu,hivyo kuelekea kwenye uchaguzi mkuu unaofanyika mwaka huu suala la amani liwe ni ajenda ya kipaumbele kwa kila mtanzania.
Chifu Wiliam Machimu Mwenyekiti wa Taasisi ya Wafikiriaji Duniani (DAWADU) amewaomba watanzania kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili waweze kuwabaini watu ambao wamekuwa wakileta taharuki na hofu ya kutoweka amani siku ya upigaji wa kura.
Machimu amesema kuwa jukumu la ulinzi na usalama ni la watanzania wote lakini ni muhimu wakapewa ushirikiano mkubwa ili waweze kuwabaini wale wote wanaotaka kuchafua sifa ya amani tuliyonayo toka tufanye changuzi zote zilizopita.
Hata hivyo amemewataka watu wenye sifa na vigezo vya kupiga kura kutumia haki yao ya kimsingi kwa kujitokeza kwa wingi kwenda kuwachagua viongozi watakaowafaa, badala ya kukaa majumbani na kulaumu kutokana na taarifa mbalimbali zinaotolewa kupitia mitandao iliyoibuka.