Dodoma FM
Dodoma FM
8 October 2025, 11:12 am

.
Wameongeza kuwa mbali na visima hivyo lakini bado wamekuwa wakitumia muda mwingi kukaa kwenye foleni kwani visima hivyo havitoi maji yakutosha.
Na Victor Chigwada.
Wananchi Kijiji Cha Mjeloo, wilaya ya Chamwino wamesema kuwa pamoja na uhaba wa huduma ya maji lakini kupitia mpango wa kusaidia kaya masikini wameweza kunufaika na visima vichache.
Wamesema hapo mwanzo walilazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya maji na maji hayo hayakua safi na salama kwa matumizi ya nyumbani. Lakini kupitia mpango wa kaya maskini umeleta unafuu kupitia visima vilivyochimbwa na TASAF.
Wameongeza kuwa mbali na visima hivyo lakini bado wamekuwa wakitumia muda mwingi kukaa kwenye foleni kwani visima hivyo havitoi maji yakutosha.
Emanueli Tanaga ni Mwenyekiti wa Mjeloo amekiri uwepo wa bwawa,mifereji na hata visima vya maji vilivyotokana na ujio wa mradi wa TASAF ambao kwa sasa umeisha kwa awamu ya kwanza.
Ikumbukwe kuwa wakazi hawa matumaini yao yapo katika mradi mkubwa wa ujenzi wa kisima cha maji kilichopo Handali ambacho mpaka sasa kimekwama mkandarasi akisubiri fedha ili kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya maji.