Dodoma FM
Dodoma FM
6 October 2025, 3:30 pm

Picha ya pamoja ya mgeni rasmi Kamanda wa Polisi jamii na wanamichezo. Picha na Selemani Kodima.
Katika Bonanza hilo ambalo limehusisha Mchezo wa mpira wa Miguu kwa kushuhudia mechi zikichezwa na baadhi ya timu zikijinyakulia zawadi mbalimbali ikiwemo Mbuzi,Vifaa vya Michezo ikiwemo Mpira pamoja na pesa Taslimu.
Na Selemani Kodima.
Imeelezwa kuwa hali ya ukuaji wa Watoto bado ni changamoto inayosababisha uwepo wa udumavu miongoni mwa watoto wenye umri wa mwaka sifuri hadi miaka nane.
Aidha hali hiyo imetajwa kusababisha uelewa mdogo wa mtoto wa kujifunza masomo akiwa shuleni.
Hayo yamesemwa na Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wilayani Bahi Songoro Msongo wakati akizungumza katika Bonanza la Michezo lililondaliwa na Jeshi la Polisi kata ya Bahi kwa kushirikiana na kanisa la FPCT kupitia mradi wa Elimu jumuishi,jamii Jumuishi.
Akizungumza na wanamichezo sambamba na wananchi wa kata hiyo ,Songoro amesema ni muhimu wazazi kutambua hatua kamili za malezi na makuzi ya mtoto tangu mimba ilipotungwa ili kufanikisha ukuaji salama kwa mtoto.
Songoro amesema ili kufanikisha hatua hiyo ni muhimu jamii kuacha kuishi kwa mazoea na kuchukua hatua kwa kila mmoja kuhudhuria kliniki ili kufahamu maendeleo ya mtoto.
Awali katika Bonanza hilo Mratibu wa Mradi wa Elimu Jumuishi kutoka FPCT Jane Mgidange ameikumbusha jamii juu kuhakikisha wana waandikisha watoto wote kwa ajili ya kupata elimu.
Aidha amesema kupitia sera ya elimu jumuishi ni muda sasa kila mtoto kupata haki ya kupata Elimu.
Nae Koplo wa Polisi kutoka Dawati la Jinsia na Watoto wilaya ya Bahi Sarah Malili na Polisi kata ya Bahi Tiimanywa wameitaka jamii ya kutambua kuwa ni wajibu wao wa Msingi kuhakikisha mtoto anapata malezi bora ya elimu sambamba na Matunzo.

Katika Bonanza hilo ambalo limehusisha Mchezo wa mpira wa Miguu kwa kushuhudia mechi zikichezwa na baadhi ya timu zikijinyakulia zawadi mbalimbali ikiwemo Mbuzi,Vifaa vya Michezo ikiwemo Mpira pamoja na pesa Taslimu.
Hata hivyo timu ya Bodaboda Bahi imefanikiwa kuwa mabingwa wa bonanza hilo huku timu ya sekondari Bahi D ikiwafungua timu ya Sekondari Bahi,Hata Hivyo bonanza hilo lilmehusisha timu za Nagulo bahi,Bodaboda,Mapawatila,wabrazili.