Dodoma FM
Dodoma FM
3 October 2025, 11:22 am

Licha ya elimu iliyotolewa mwanzoni mwa mpango huo lakini bado haikueleweka kwa wananchi wengi.
Na Victor Chigwada.
Wakazi wa Kijiji cha Chanhumba Kata ya Handali Wilaya ya Chamwino wamesema imekuwa ni vigumu kupokea zoezi la urasimishaji wa ardhi kwa kuhofia malipo ya kodi ya ardhi kwamba inaweza kupelekea wao kupoteza haki ya umiliki wa maeneo yao.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Ndg.Amos Lusiji na kusema kuwa licha ya elimu iliyotolewa mwanzoni mwa mpango huo lakini bado haikueleweka kwa wananchi wengi.
Lusiji ameongeza kuwa wananchi wengi wanahofia kudhurumiwa huku baadhi yao wakiona ni vigumu kuruhus maeneo yao kupotea kwani hawaoni fedha za kulipia serikalini.
Aidha pamoja na changamoto hiyo Lusiji ameiomba serikali kuendelea kupeleka waatalamu wa ardhi ili kutoa elimu zaidi kwa wananchi.
Nao baadhi ya wananchi wameonyesha kuwa na uelewa mdogo juu ya zoezi la urasimishaji wa ardhi kwani wanacho kiona ni kama wanapelekwa kwenye mfumo wa wao kununua ardhi yao.
Hata hivyo wameitaka mamlaka husika kufika katika mikutano na kutoa elimu itakayowawezesha wananchi waweze kuwashawishi kuingia katika mfumo wa hati miliki