Dodoma FM
Dodoma FM
1 October 2025, 4:21 pm

Sheria ya Wenye Nyumba na Wapangaji – Toleo la 2009) ya Tanzania lengo lake ni kuhakikisha uwiano wa haki na wajibu kati ya mwenye nyumba na mpangaji, kuzuia migogoro, na kutoa mfumo wa kisheria wa kutatua mizozo ya upangaji. Picha na Dodoma FM.
Sheria za nyumba Tanzania zinahakikisha uwiano kati ya haki za mmiliki na mpangaji, zikilenga kuepuka migogoro na kuhakikisha makubaliano ya kisheria yanatekelezwa.
Na Joseph Gontako
Wamiliki wa nyumba na wapangaji wametakiwa kuhakikisha kwamba mikataba ya upangaji inazingatiwa kikamilifu, ili kuepuka migogoro ya baadaye inayohusiana na kodi ya nyumba.
Hayo yamebainishwa na Kajetan Tumain, mtaalamu wa sheria za makazi, wakati akizungumza na Taswira ya habari ambapo amebainisha kuwa migogoro mingi hutokea pale ambapo upandishaji wa kodi hauzingatii makubaliano ya mkataba au ambapo wapangaji hawajafahamishwa vyema kuhusu mabadiliko hayo.
Sanjari na hayo, Tumain amewataka wapangaji wajiridhishe na makubaliano ya mkataba kabla ya kufanya marekebisho yoyote, ili kuepuka mizozo isiyohitajika.
Sauti ya Kajetan Tumaini.