Dodoma FM
Dodoma FM
1 October 2025, 12:04 pm

Wamesema hali hiyo imewavunja moyo kuendelea kutumikia wananchi bila malipo ya kifuta jasho.
Wanaiomba serikali kuwatambua kama sehemu ya ngazi za uongozi na kuwapa posho za kila mwezi. Picha na Blogsport.
Kilio hiki cha wenyeviti kukosa mishahara au kifuta jasho kimeendelea kwa miaka mingi, licha ya mara kadhaa serikali kuu kuahidi kuanza kuwalipa posho za kila mwezi.
Na Victor Chigwada.
Imeelezwa kuwa kukosekana kwa viinua mgongo na mishahara kwa wenyeviti wa vijiji na mitaa kimekuwa chanzo kikuu cha kuwavunja mioyo viongozi hao katika utendaji wao wa kazi.
Kilio hiki cha wenyeviti kukosa mishahara au kifuta jasho kimeendelea kwa miaka mingi, licha ya mara kadhaa serikali kuu kuahidi kuanza kuwalipa posho za kila mwezi.

Atanasio Mnyepembe, Mwenyekiti wa Kijiji cha Idifu, amesema kuwa licha ya shina la serikali kuanzia ngazi ya kijiji, wao wamekuwa hawatambuliki kama viongozi vingine.
Amesema kuwa viongozi wengi wemevunjika mioyo ya kuendelea kujitolea bila malipo, kwani viongozi wote kwa asilimia kubwa wanalipwa ikiwa sambamba na viongozi wa chama.
Aidha, Mwenyekiti wa Kijiji cha Muungano, Ndg. Matonya Mtukamsihi, amesema kuwa kwa upande wa Jimbo la Mvumi Makulu, licha ya kuambiwa kufungua akaunti, hadi sasa walifanikiwa kuingiziwa posho ya mwezi mmoja tu.
Mtukamsihi ameiomba serikali kuwakumbuka kwani wao ni sehemu ya serikali na wanafanya kazi nyingi kwa uzalendo; hivyo ni vyema kuwafikilia kwa kina.