Dodoma FM

RUWASA yaombwa kuboresha miundombinu ya maji Iwondo

30 September 2025, 12:53 pm

Iwapo visima hivyo vingeboreshewa na kuongezewa nguvu ya umeme, vingeweza kuhudumia wananchi wengi zaidi.Picha na Ruwasa.

Changamoto kubwa ni kukosekana kwa umeme wa kutosha wa kusukuma mashine za visima vilivyopo.

Na Victor Chigwada.
Wananchi wa kijiji cha Iwondo, Kata ya Dabalo, Wilaya ya Chamwino wameiomba Mamlaka ya Usimamizi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kuboresha miundombinu ya maji ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa huduma hiyo.

Wakizungumza na Dodoma FM, wananchi wamesema licha ya jitihada zilizopo, changamoto kubwa ni kukosekana kwa umeme wa kutosha wa kusukuma mashine za visima vilivyopo.

Wameeleza kuwa iwapo visima hivyo vingeboreshewa na kuongezewa nguvu ya umeme, vingeweza kuhudumia wananchi wengi zaidi tofauti na sasa ambapo mara kwa mara huduma hiyo hukatika na kuwalazimu kutumia maji ya visima vya asili.

Sauti za wananchi

Akizungumzia hali hiyo, Idadi Magoti, Mhandisi wa Maji RUWASA Wilaya ya Chamwino amesema jukumu la msingi la RUWASA ni kuchimba visima na kuweka miundombinu ya maji, lakini suala la nishati ya umeme halipo chini ya mamlaka hiyo.

Sauti ya Idadi Magoti,