Dodoma FM
Dodoma FM
26 September 2025, 2:14 pm

Msikilizaji, leo tunazungumzia Kutotekelezwa kwa sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 sura 20 kufungu cha 114-116 kumesababisha kulundikana kwa taka za majumbani katika mitaa ya Chanagnyikeni, Kibaoni na St Gemma katika kata ya Miyuji Jijini Dodoma.
Na Mariam Kasawa.
Karibu msikilizaji wa Dodoma FM katika makala ya Amua, makala hii imeandaliwa na Mariam Kasawa na kutangazwa na Dodoma FM…
Katika Makala hii tunaangazia kutotekelezwa kwa sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 sura 20 kufungu cha 114-116 kulivyosababisha mrundikano wa taka za majumbani katika mitaa ya Chanagnyikeni, Kibaoni na St. Gemma katika kata ya Miyuji Jijini Dodoma.
Mlundikano wa taka katika mitaa ya Changanyikeni, Kibaoni na St. Gemma katika kata ya Miyuji Jijini Dodoma unakinzana na matakwa ya Sheria ya Mazingira ya waka 2004 (sura na 20) kifungu cha 114-116. Wakati wananchi wa mitaa mingine wanaishi katika hali takiwa kwa kuweka utaratibu mzuri wa kudhibiti kuzagaa kwa taka ngumu za majumbani kwa gari la taka kupita kila wiki na wananchi kuchangia gharama za kumlipa mzabuni kila mwezi, mitaa hii mitatu hali ni tofauti.
Uchunguzi wa awali umebaini kwamba viongozi wa mitaa hii wameshindwa kushirikiana na wa ngazi ya halmashauri na kuwaandalia wananchi utaratibu, ukiwemo kuwatafutia wazabuni wanaotoza huduma ya uzoaji taka gharama nafuu.

Hali hii imefanya jukumu la uzoaji na utupapaji wa taka kuwa ni la kila mtu na kila kaya. Matokeo yake ni mifuko yenye taka ngumu zikiwemo zilizooza, kujaa vichochoroni, mitaroni, pembezoni mwa barabara na hata sehemu za wazi wanakocheza watoto.
Hii ni kinyume na muongozo wa serikali wa kupendezesha miji na majiji kwa kuiweka safi na kupanda miti pembezoni mwa barabara, uliotangazwa na Makamu wa Rais Dk Philip Mpango mwaka 2023. Muongozo huu umetanfazwa na serikali mwaka huu kama sehemu ya upimaji wa ufanisi (key performance indicator) kwa watendaji wa mamlaka za miji na majiji.