Dodoma FM

Wananchi watakiwa kuzingatia sheria ya mirathi

24 September 2025, 6:28 pm

Changamoto kubwa katika familia nyingi ni kutoandikwa kwa wosia, jambo linalosababisha migongano.Picha na Mwanasheria.

Komba ameitaka jamii kwa ujumla kutafuta ushauri wa kisheria mapema wanapokutana na changamoto zinazohusiana na mirathi, ili kuhakikisha haki za warithi zinatimizwa na mgogoro wowote unatatuliwa kwa mujibu wa sheria.

Na Joseph Julius.
Wananchi jijini Dodoma wametakiwa kuzingatia masharti ya sheria ya mirathi na urithi wa mali ili kuepusha migogoro ya kifamilia inayojitokeza baada ya kifo cha wapendwa wao.

Akizungumza na Taswira ya habari Betram Komba ambaye ni Mwanasheria kutoka kampuni ya Law Age Consult and Advocates, amesema kuwa changamoto kubwa katika familia nyingi ni kutoandikwa kwa wosia, jambo linalosababisha migongano kati ya ndugu, jamaa na marafiki baada ya msiba.

Aidha, Komba amefafanua kuwa sheria ya mirathi inatambua urithi wa mali kupitia taratibu rasmi, ambazo zinahusisha,uteuzi wa wasimamizi wa mirathi, uhakiki wa mali na madeni ya marehemu, na hatimaye mgawanyo wa mali kwa warithi halali.

Sauti ya Betram Komba

Amesisitiza kwamba jamii inapaswa kuelewa haki zao kisheria ili kupunguza migogoro inayotokea kutokana na urithi.

Aidha, ameeleza kuwa mwanasheria anaweza kusaidia familia katika kupanga mirathi kwa usahihi, kuhakikisha haki za kila mrithi zinatimizwa na mali za marehemu zinagawanywa kwa mujibu wa sheria.