Dodoma FM

Bodaboda watakiwa kujiunga na vyama vya wafanyakazi

24 September 2025, 6:06 pm

Maafisa usafirishaji wanaojulikana kama bodaboda ni sekta isiyo rasmi ambayo imekuwa tegemeo muhimu zaidi kwa vijana.Picha na Jambo

Maafisa usafirishaji wametakiwa kuhakikisha wanapata vitambulisho vya kidijitali vya wafanyabiashara wadogo ili kuwasaidia kupangiwa maeneo rasmi ya kufanyia kazi.

Na Lilian Leopold.
Zaidi ya vijana 23,000 jijini Dodoma wanajipatia kipato cha kila siku kupitia uendeshaji wa pikipiki na bajaji .

Wakizungumza katika kikao cha Maafisa Usafirishaji na Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano na Uchukuzi COTWU (T), washiriki wakiwemo maafisa wa maendeleo ya jiji na mashirika ya kimataifa wamesema sekta hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa maeneo rasmi yaliyopangwa kwa ajili ya kuegesha vyombo vyao.

Akizungumza baada ya kikao hicho, Mtafiti wa COTWU (T), Nice Mwasasu, amesema ili kukabiliana na changamoto hizo, maafisa usafirishaji hawana budi kujiunga katika vyama vya wafanyakazi, kwani vyama hivyo vitwasaidia kulinda usalama wao.

Sauti ya Nice Mwasasu,

Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jiji la Dodoma, Bw. Patrick Sebiga, amewataka maafisa usafirishaji kuhakikisha wanapata vitambulisho vya kidijitali vya wafanyabiashara wadogo ili kuwasaidia kupangiwa maeneo rasmi ya kufanyia kazi.

Sauti ya Bw. Patrick Sebiga.