Dodoma FM
Dodoma FM
23 September 2025, 4:27 pm

Wamesema kuwa hata kama barabara hizo hazijawekewa kiwango cha lami, ni vyema kujengewa mifereji pembezoni ili maji yatiririke kwa urahisi.
Na Victor Chigwada.
Imeelezwa kuwa mvua pamoja na maji yanayotiririka yamekuwa changamoto kubwa kwa barabara za vijijini, kutokana na vifusi vinavyotumika kuwa vya udongo ambavyo hubebwa na maji mara tu mvua inaponyesha.
Wakazi wa Kijiji cha Mlazo, Kata ya Ngh’ambaku, wameiomba Serikali kuboresha miundombinu ya kuelekeza maji, hususan katika barabara zilizopo maeneo ya mwinuko, ili kuepusha maji yasiharibu barabara.
Wameeleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuepuka madhara ya barabara kujaa madimbwi, hali inayosababisha ugumu wa huduma za usafirishaji na hivyo kukwamisha shughuli mbalimbali, sambamba na kuhatarisha maisha na makazi ya wananchi.