Dodoma FM
Dodoma FM
22 September 2025, 4:53 pm

Hata hivyo, wanasema kuwa tofauti hiyo haizuizi kupata msaada wa kitaaluma na kuendelea kukuza elimu yao pasipo mashaka.
Na Victor Chigwada .
Imeelezwa kuwa tofauti za mfumo wa elimu ya juu na ule wa msingi na sekondari zimekuwa changamoto kwa baadhi ya vijana pindi wanapojiunga na masomo mapya chuoni, hususan katika kutumia vifaa vya kielimu kama projekta na mbao za makapeni.
Wameeleza kuwa muundo wa shule za msingi na sekondari unawasaidia wanafunzi kuzoea mafunzo ya msingi, jambo ambalo linakuwa tatizo wanapofika chuoni kwani hutokea kushindwa kukabiliana na mwanga wa projekta na utumiaji wa ubao wa makapeni.
Aidha, wamesema changamoto nyingine inatokana na shule za ngazi ya chini kukosa baadhi ya vifaa vinavyohitajika kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu. Hali hiyo inawafanya kuumia pale wanapopata fursa za kujiunga na masomo ya vyuo vikuu, kwani vifaa vingi vinakuwa vigeni kwa namna ya matumizi.