Dodoma FM

Mkutano wa klabu za wasichana Amani wafanyika Dodoma

22 September 2025, 2:20 pm

Picha ni Mkutano wa pili wa mwaka wa walezi wa Klabu za Msichana Amani ambao umefanyika jijini Dodoma, na kuwakutanisha walimu 164. Picha na Seleman Kodima.

Walimu kutoka mikoa minne tofauti hapa Tanzania, walieleza furaha yao juu ya kuhusika katika mkutano huo na kuelezea namna wanavyonufaika na programu hii.

Na Seleman Kodima.
Mkutano wa pili wa mwaka wa walezi wa Klabu za Msichana Amani umefanyika jijini Dodoma, na kuwakutanisha walimu 164 kutoka mikoa ya Dodoma, Tabora, Bagamoyo na Dar es Salaam.

Lengo kuu la mkutano huu ni kuwaunganisha walezi wa klabu hizo ili kujifunza kwa pamoja, na kujenga mtandao wa mshikamano katika malezi ya mtoto wa kike na kiume mashuleni.

Kwa upande wake, Afisa Miradi wa Taasisi ya Klabu za Wasichana Amani, Steven Kiboko, alizungumzia umuhimu wa taasisi hiyo na mchango wake katika kuleta mabadiliko chanya kwa watoto wa kike.

Picha ni Mkutano wa pili wa mwaka wa walezi wa Klabu za Msichana Amani ambao umefanyika jijini Dodoma, na kuwakutanisha walimu 164. Picha na Seleman Kodima.
Sauti ya Amani Steven Kiboko.

Aidha, washiriki wa mkutano huo ambao ni walimu kutoka mikoa minne tofauti hapa Tanzania, walieleza furaha yao juu ya kuhusika katika mkutano huo na kuelezea namna wanavyonufaika na programu hii.

Sauti za washirika.