Dodoma FM
Dodoma FM
18 September 2025, 1:58 pm

Waandishi wa habari wametakiwa kutambua kuwa wana haki ya kuripoti habari zote za uchaguzi bila ubaguzi wowote.
Na Mariam Kasawa.
Tume ya haki za binadamu na utawala bora imewataka waandishi wa habari kuzingatia maadili kuepuka lugha za matusi, takrima na vurugu katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu unao tarajia kufanyika octoba 29.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu na utawala bora Jaji Mstaafu Mh. Mathew Mwalimu alipokuwa akifungua mafunzo yaliyo tolewa na tume hiyo kwa waandhishi wa habari jijini Dodoma.
Aidha amewataka waandishi wa habari kutambua kuwa wana haki ya kuripoti habari zote za uchaguzi bila ubaguzi wowote.