Dodoma FM
Dodoma FM
16 September 2025, 3:33 pm

Lengo kuu ni kuongeza uelewa na matumizi ya teknolojia ya Akili unde katika shughuli za maendeleo nchini.
Na Seleman Kodima.
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimezindua rasmi mafunzo ya Akili Unde(AI), kwa kushirikisha wanafunzi pamoja na taasisi mbalimbali kutoka sekta binafsi na za umma.
Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Khamis Abdulla, amekipongeza Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kuandaa na kuendesha mafunzo hayo muhimu ya Akili unde. Aidha, ameyataka vyuo vingine nchini kuiga mfano huo kwa kuandaa mafunzo yanayolenga kukuza maarifa ya teknolojia mpya miongoni mwa vijana.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi, Dkt. Mohammed Mjahidi, amesema kuwa mafunzo hayo yamewahusisha washiriki kutoka makundi mbalimbali, wakiwemo wanafunzi wa vyuo vikuu, pamoja na wawakilishi kutoka taasisi za umma na binafsi.
