Dodoma FM

Ndogowe waiomba serikali kukamilisha uchimbaji wa kisima

16 September 2025, 2:27 pm

Wakazi hao wameiomba serikali kutimiza ahadi ya uchimbaji wa kisima na bwawa kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji.Picha na Blog sport.

Serikali iliweka ahadi ya kuchimba kisima sambamba na ujenzi wa bwawa ambalo litawanufaisha wakazi wa eneo hilo Kwa kilimo cha umwagiliaji lakini bado haijateleza ahadi hiyo hadi leo.

Na Victor Chigwada.
Wakazi wa Kijiji cha Ndogowe Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wameiomba serikali kukamilisha uchimbaji wa kisima pamoja na bwawa la kilimo cha umwagiliaji ndani ya kata yao.

Kenneth Muhawi mwenyekiti wa kijiji hicho amekiri uwepo wa ahadi ya kuchimbiwa kisima sambamba na ujenzi wa bwawa ambalo litawanufaisha wakazi wa eneo hilo Kwa kilimo.

Muhawi amesema kuwa mpaka Sasa hakuna hatua zilizo chukuliwa hivyo kuwa na mipango ya kufuatilia ahadi hizo katika mamlaka husika.

Sauti ya Kenneth Muhawi

Nao baadhi ya wananchi wameipongeza Serikali kuhakikisha inatekeleza Miradi mbalimbali.
Aidha wameiomba kuikamilisha miradi ya kisima na bwawa katika Kijiji Chao Ili kuendelea kuwanufaisha wananchi wa Ndogowe.

Sauti za wananchi.