Dodoma FM

Teknolojia inavyoathiri malezi ya watoto

15 September 2025, 3:52 pm

Matumizi ya simu janja na intaneti yamechangia kuporomoka kwa malezi ya baadhi ya watoto.Picha na google.

Teknolojia inaweza kuwa chachu ya maendeleo ikiwa itatumika kwa uangalifu na kwa ushauri wa karibu kutoka kwa wazazi.

Na Joseph Gontako.
Imeelezwa kuwa mabadiliko ya kiteknolojia yameathiri mfumo wa malezi katika jamii, kutokana na baadhi ya wazazi kutumia teknolojia zaidi katika malezi ya watoto.

Hayo yamebainishwa na Mtaalamu wa masuala ya saikolojia, Madam Muhele, wakati akizungumza na Taswira ya Habari, ambapo amesema matumizi ya simu janja na intaneti yamechangia kuporomoka kwa malezi ya baadhi ya watoto. Wazazi wengi hukosa muda wa kuwa karibu na watoto wao na badala yake kutumia teknolojia kama njia mbadala ya kuwaelekeza.

Sauti yaMadam Muhele.

Madam Muhele ameongeza kuwa madhara mengine yanayohusiana na malezi haya ni pamoja na kuongezeka kwa utovu wa nidhamu miongoni mwa watoto, kushuka kwa uwezo wa kitaaluma na baadhi ya watoto kujiingiza katika vitendo vya uhalifu kutokana na ukosefu wa uangalizi wa karibu kutoka kwa wazazi.

Sanjari na hayo, ametaka wazazi na walezi kutambua wajibu wao wa msingi na kuimarisha uhusiano na watoto wao ili kuhakikisha misingi ya maadili na utu inajengwa.