Dodoma FM
Dodoma FM
15 September 2025, 1:26 pm

Na Yussuph Hassan.
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini TMA imesema katika msimu wa vuli mwaka 2025 mvua zinaratajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani katika maeneo mengi na kutawaliwa na vipindi virefu vya ukavu hususan katika maeneo ya Pwani ya Kaskazini na Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki.
Imesema mvua hizo zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Novemba 2025 katika maeneo ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki na Pwani ya Kaskazini na zinatarajiwa kuisha mwezi Januari, 2026 katika maeneo mengi.
Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi Dkt. Ladislaus Chan’ga wakati akitoa taarifa kuhusu mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2025.