Dodoma FM
Dodoma FM
15 September 2025, 12:46 pm

Licha ya wananchi hao kutumia mafuta ya dizeli kukabiliana na changamoto ya umeme bado mafuta hayo hayakidhi mahitaji yao.
Na; Victor chigwada.
Imeelezwa kuwa matumizi ya mafuta ya Diesel Kwa wakazi wa Kijiji Cha Ngh’ambaku Wilaya ya Chamwino imekuwa ni changamoto kubwa Kwa wananchi kwani hayakidhi mahitaji zaidi ya kuwaumiza watumiaji.
Wamesema changamoto hiyo ya bei inachangiwa na matumizi ya mafuta katika mashine jambo ambalo linahitaji kutatuliwa Kwa kufungwa nishati ya umeme.
Mwenyekiti wa Kijiji Cha Ngh’ambaku Bw.Juma Muyeya amesema kuwa wakazi wa Kijiji hicho wanakumbana na adha ya maji kwani kisima Chao kimatumia mfumo wa mafuta ya diesel.
Muyeyu ameongeza ni vyema Serikali kutatua changamoto hiyo Kwa kupeleka nishati ya umeme kwenye kisima Cha maji kwani tofauti na hivyo kisima hicho kinawaumiza wananchi hususani wafugaji.