Dodoma FM
Dodoma FM
10 September 2025, 4:03 pm

Hata hivyo juhudi za kumpata meneja TANROAD Wilaya ya Chamwino hazikuweza kufanikiwa.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa Kijiji cha Ndogowe Kata ya Ngh’ambaku Wilaya ya Chamwino wameeleza kilio chao uchakavu wa barabara hali inayokwamisha huduma za usafirishaji kwa wananchi.
Wamesema barabara inayotoka Kijiji kwao kwenda sehemu maeneo mengine huku adha ikiwaathiri zaidi wamama wajawazito pindi wanapohitaji kufika vituo vya afya.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Ndg.Keneth Muhawi amesema kuwa barabara yao imekuwa ikiwawia vigumu kusafiri Kwa uhakika hususani linapokuja suala la kusafirisha mgonjwa.
Muhawi amesema kumekuwa na uharibifu mkubwa kwenye maeneo yenye makorongo sambamba na mawe mengi barabarani.
Aidha ameiomba Serikali kutekeleza ahadi ya kufanya ujenzi wa barabara hiyo kupitia wakala wa barabara kuu TANROAD.