Dodoma FM

Mafunzo ya kanzi data yafanyika kuboresha ukusanyaji mapato

2 September 2025, 4:12 pm

Picha ni Akida Hudu, Muhasibu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma akiongea wakati wa mafunzo hayo .Picha na jiji la Dodoma .

Na Lilian Leopold.

Mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kanzi data kwa watumishi wa Kanda sita za utoaji hudumawamefanyika chini ya usimamizi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kwa lengo la kuboresha ukusanyaji wa mapato.

Akida Hudu, Muhasibu wa Halmashauri hiyo, ameonyesha umuhimu wa mfumo huu wakati akiwafundisha watumishi juu ya matumizi ya mfumo huo. Amevitaja vyanzo kadhaa ambavyo mfumo utafungua njia ya ukusanyaji wa mapato kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na huduma mbalimbali, leseni za biashara, ushuru wa mabango, naajibika kwa vizimba.

Sauti ya Bw. Akida Hudu

Kwa upande wake, Lucas Nkelege, Meneja wa Kanda namba sita, amebainisha kwamba mafunzo haya yatawezesha ufanisi mkubwa katika ukusanyaji wa mapato kutoka vyanzo mbalimbali, jambo litakalovutiana kuharakisha utekelezaji wamiradi ya maendeleo ya jiji.

Sauti ya Lucas Nkelege
Picha ni Mafunzo ya matumizi ya mfumo wa kanzi data kwa watumishi wa Kanda sita za utoaji huduma.Picha na jiji la Dodoma.

Baadhi ya watumishi waliohudhuria mafunzo hayo, wameeleza kwamba mfumo huo wa kanzi data utarahisishia wananchi kupata huduma kwa urahisi na kwa haraka kuliko awali.

Sauti za baadhi ya watumishi.

Katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, mfumo wa kanzi data unalenga kuunganisha vyanzo mbalimbali vya ukusanyaji mapato kama huduma, leseni za biashara, ushuru wa mabango, kodi za nyumba na vizimba. Hii inalenga kuharakisha mchakato na kupunguza matatizo.