Dodoma FM
Dodoma FM
1 September 2025, 2:20 pm

Maadhimisho hayo yalihusisha utoaji zawadi kwa kata zilizofanya vizuri katika robo mwaka, pamoja na elimu ya kilimo na afya ya akili, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Alhaj Jabir Shekimweri.
Na Lilian Leopold
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri, amewataka wazazi kuhakikisha wanazingatia malezi bora ya mtoto kuanzia akiwa tumboni, akisisitiza umuhimu wa ufuatiliaji wa afya, lishe na kujenga msingi imara kabla ya kuzaliwa.
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe yaliyofanyika kata ya Mnadani, Alhaj Shekimweri amesema malezi ya mtoto hayawezi kuanza baada ya kuzaliwa pekee, bali ni lazima yaanze akiwa tumboni, kipindi ambacho mama huhitaji uangalizi maalum.
Kwa upande wao, baadhi ya wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo wamesema elimu waliyoipata imewasaidia kuelewa namna ya kuboresha afya ya mama na mtoto, na wameahidi kuyafanyia kazi kwa manufaa ya familia na jamii kwa ujumla.
