Dodoma FM
Dodoma FM
29 August 2025, 3:47 pm

watatumia maadhimisho hayo kutembelea vituo vya awali na vya kulelea watoto kwa ajili ya kutoa elimu ya makuzi.
Na lilian Leopold.
Wiki ya Ustawi wa Jamii imeanza kuadhimishwa rasmi hapa nchini, huku Jiji la Dodoma likitumia fursa hiyo kutoa elimu ya malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto kwa wakina mama.
Akizungumza na waandishi wa habari Afisa Ustawi jiji la Dodoma Leila Mbinga amesema watatumia maadhimisho hayo kutembelea vituo vya awali na vya kulelea watoto kwa ajili ya kutoa elimu ya makuzi kwa mtoto.