Dodoma FM

TAMESO (T) yawataka waganga wa tiba asili kushiriki mafunzo

25 August 2025, 3:48 pm

Waganga wa tiba asili na tiba mbadala wanatakiwa kujisajili ndani ya mfumo rasmi.Picha na google.

Mafunzo hayo ni muhimu na yanalenga kuimarisha uelewa, uhifadhi wa maadili na usalama katika utoaji wa huduma za tiba asili.

Na. Lilian Leopold.
Wito umetolewa kwa waganga wa tiba asili na tiba mbadala kushiriki kikamilifu kwenye vikao maalum na mafunzo yanayoandaliwa na TAMESO T yaani Traditional and Alternative Medicine Socity of Tanzania.
Hii inajili baada ya tukio la kusikitisha lililotokea Agosti 16, 2025 katika kata ya Qashi, ambapo ramli chonganishi ilisababisha kifo cha mtu asiye na hatia, tukio lililotia hofu na kutia mashaka uaminifu na usalama wa tiba za asili.

Akizungumza na Taswira ya habari Katibu Mkuu wa Chama Cha TAMESO T Lucas Joseph Mlipu kutoka Makao Makuu ya Mamlaka ya Mji mdogo wa Kibaigwa mkoa wa Dodoma amesema mafunzo hayo ni muhimu na yanalenga kuimarisha uelewa, uhifadhi wa maadili na usalama katika utoaji wa huduma za tiba asili.

Sauti ya Joseph Mlipu.

Aidha amewataka waaganga wa tiba asili na tiba mbadala kujisajili ndani ya mfumo wake rasmi, kama sehemu ya jitihada za kuhakikisha usalama, uadilifu na utambulisho wa kitaaluma katika utoaji huduma.

Sauti ya Joseph Mlipu.

Nao baadhi ya wananchi kutoka eneo la Mipango wamesema ramli chonganishi zimekuwa zikiharibu misingi ya imani na muungano ndani ya familia na jamii.

Sauti za wananchi.

Kwa mujibu wa Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala ya mwaka 2002 (Sheria Na. 23), serikali iliweka msingi thabiti wa kisheria kwa kuanzisha Traditional and Alternative Health Practice Council (TAHPC), yenye jukumu la kusimamia na kudhibiti taaluma ya tiba asili na tiba mbadala ikiwa ni pamoja na usajili, ufuatiliaji, na utoaji cheti kinachotambulika kote nchini.