Dodoma FM
Dodoma FM
25 August 2025, 2:05 pm

Amemtaka mkurugenzi wa jiji kushirikiana na Bodi ya Utalii kuangalia namna ya kuifanya Stesheni ya Treni ya SGR kuwa kivutio cha utalii.
Na Peter Nnunduma.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Suleman Jafo, ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kuanzisha kijiji cha utalii wa Wagogo, ikiwa ni mkakati wa kuimarisha sekta ya utalii katika mkoa huo.
Agizo hilo amelitoa katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha mikakati ya ukuzaji wa utalii ndani ya Jiji la Dodoma, iliyofanyika katika ukumbi wa Mabeyo.
Waziri Jafo amesema ni muhimu kwa serikali ya mkoa wa Dodoma kubuni vivutio vya kipekee vya utalii na kutumia fursa ya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi kama njia ya kuvutia watalii wa ndani na nje.