Dodoma FM
Dodoma FM
25 August 2025, 1:42 pm

Mbali na hayo ASP Christer Kayombo amesema kuwa madeni yaliyopitiliza yanaweza kusababisha Mzazi kujiingiza katika biashara zisizofaa na kuathiri mwenendo mzima wa maisha ya mtoto.
Na Farashuu Abdallah.
Imeelezwa kuwa madeni yaliyopitiliza kwa Wazazi ni chanzo cha kuathiri ukuaji wa Mtoto katika nyanja mbalimbali.
Mrakibu msaidizi wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Dawati la jinsia Mkoa wa Dodoma ASP Christer Kayombo ameyasema hayo wakati akizungumza na Dodoma Fm ambapo amesema wingi wa madeni ya wazazi yanaweza kumuathiri Mtoto kiuchumi, kielimu, kisaikolojia na hata kuathiri Afya ya Mtoto.
Aidha ametoa wito kwa wazazi juu ya kuepuka madeni yasiyo na ulazima ambayo yatasababisha athari za familia.