Dodoma FM
Dodoma FM
22 August 2025, 1:31 pm

Picha ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dt. Dotto Biteko na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakiwa na wafanyabiashara wa nyama choma Msalato. Picha na Seleman Kodima.
Katika kuhakikisha watanzania 80% wanatumia nishati safi ya kupikia Naibu Waziri Mkuu Dkt.Dotto Mashaka Biteko agosti 21 amekutana na wachoma nyama Mnadani Msalato.
Na Seleman Kodima.
Katika kuhakikisha watanzania 80% wanatumia nishati safi ya kupikia Naibu Waziri Mkuu Dkt.Dotto Mashaka Biteko Agosti 21 amekutana na wachoma nyama Mnadani Msalato.
Akizungumza na wanachi,wadau na wachoma nyama Dkt. Biteko amewataka kutumia nishati safi ya kupikia kwenye matumizi ya uchomaji nyama .

Aidha kwa upande mwingine Daktari Biteko amewataka wananchi,wadau na wachoma nyama kuweza kulinda minada ya nyama.
Ikumbukwe matumizi bora ya nishati safi ya kupikia ni sera ya Rais Daktari Samia Suluhu Hassan ,ifikapo 2034 kila mtanzania awe anatumia nishati safi ya kupikia.