Dodoma FM
Dodoma FM
21 August 2025, 4:09 pm

Alhaj Jabir Shekimweri amewasistiza walimu kuwa ajenda ya lishe shuleni iwe endelevu na kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanapata chakula.
Na Lilian Leopold.
Katika juhudi za kuboresha elimu na afya ya wanafunzi, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Alhaj Jabir Shekimweri, amesema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaendelea kutekeza agizo la Rais kuwa watoto ni kipaumbele cha kwanza kupata chakula wakiwa shuleni.
Ameyabainisha hayo mara baada ya kutembelea Shule ya Msingi Kizota, August 20,2025 kwa lengo la kukagua utekelezaji wa ajenda ya lishe shuleni.

Kwa upande wao Afisa lishe wa Jiji la Dodoma, Alfa Fanuel na Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Kizota Hamida Mkingule wamesema kupitia utekelezaji wa agenda ya lishe shuleni umesaidia kupunguza utoro shuleni na kuwasaidia wanafunzi kushiriki kikamilifu katika masomo na michezo.