Dodoma FM
Dodoma FM
20 August 2025, 5:13 pm

Kupitia mafunzo hayo, vijana wa skauti wanatarajiwa kuwa mabalozi wa uokoaji na usalama wa jamii katika maeneo yao, wakihamasisha pia elimu ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga mbalimbali.
Na Anwary Shaban.
Ili kukabiliana na majanga mbalimbali pindi yanapotokea, Chama cha Skauti Tanzania kimetoa mafunzo yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kutoa msaada kwa jamii na kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.
Akizungumza jijini Dodoma wakati wa utoaji wa mafunzo hayo, Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania, Luteni Abubakari Mtitu, amesema elimu hiyo ni muhimu kwa vijana hao kwani inawasaidia kubadilika kimtazamo na kujifunza kutoa taarifa mapema za majanga pamoja na kushiriki kikamilifu katika kusaidia jamii badala ya kuwaachia tu vyombo vya uokoaji kama Jeshi la Zimamoto.
Aidha, Kamishna Mtitu ameongeza kuwa elimu hiyo itawasaidia vijana hao kuwa mstari wa mbele katika kuisaidia jamii wakati wa majanga, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sahihi kwa mamlaka husika.