Dodoma FM
Dodoma FM
19 August 2025, 3:13 pm

Ikumbukwe kuwa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge na urais zitafanyika kuanzia Agosti 28 hadi Oktoba 28, siku inayofuata Jumatano, Oktoba 29, 2025 itakuwa siku ya upigaji kura.
Na Farashuu Abdallah.
Vyama vya siasa vimetakiwa kufanya siasa za kiusataarabu katika kipindi hiki cha kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa Octoba 2025.
Wito huo umetolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi kwenye mafunzo kuhusu sheria ya gharama za uchaguzi katika ukumbi wa JNICC Mkoani Dar es salaam.
Jaji Mutungi amesema ni muhimu kwa viongozi kujiepusha na lugha ya matusi,uchochezi na kashfa katika kampeni zao.
Pia amesisitiza vyama vya siasa viwe mabalozi wa kuimarisha amani na mshikamano katika Taifa.

Ikumbukwe kuwa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge na urais zitafanyika kuanzia Agosti 28 hadi Oktoba 28, siku inayofuata Jumatano, Oktoba 29, 2025 itakuwa siku ya upigaji kura.
Kwa sasa vyama 18 vinavyoshiriki uchaguzi huo, vinaandaa wagombea wa nafasi hizo. Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imekwisha fungua dirisha la uchukuaji na urejeshaji fomu hizo.
Uchukuaji wa fomu za uteuzi wa urais ulianza Agosti 9 hadi Agosti 27, 2025 huku ubunge na udiwani limefunguliwa kuanzia Agosti 14 hadi Agosti 27, 2025.