Dodoma FM
Dodoma FM
18 August 2025, 12:48 pm

Fursa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia itawapunguzia wanawake kutumia muda mrefu wa kutafuta kuni kwaajili ya kupikia.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa vitongoji vya Sokoine na Malechela wameiomba Serikali kuwakumbuka katika miradi ya uhamasishaji wa matumizi ya Nishati mbadala kama amabavyo baadhi ya maeneo wananufaika na mpango huo.
wamesema kupitia mpango huo itawapa fursa wananchi wa vijijini kuacha kuharibu mazingira kwa kukata miti kwaajili ya matumizi ya kuni.
Aidha wamesema kuwa fursa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia itawapunguzia wanawake kutumia muda mrefu wa kutafuta kuni kwaajili ya kupikia.
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Mnase Ayubu Malima amesema kuwa ili kukabiliana na changamoto ya uvamizi wa mazingira wameendelea kutoa elimu kwa wananchi