Dodoma FM

DUWASA yakamilisha zoezi la ulipaji fidia

14 August 2025, 6:18 pm

Picha na Afisa Mazingira kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Ambrosi Siril akimsaidia Bibi Anna Masaka kusaini katika daftari la fidia katika eneo la Zuzu Nala jijini Dodoma.Picha na DUWASA.

Baadhi ya maeneo hayo ni pamoja na Nzuguni, Zuzu Nala, Nala Chihoni na Kibaigwa.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya Maji, imekamilisha zoezi la ulipaji wa fidia yenye jumla ya Shilingi Milioni 999 kwa wananchi 103 ambao ardhi yao ilitwaliwa kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA).

Aidha Ulipaji wa fidia hizo, umeongozwa na Wizara ya Maji kwa kushirikiana na DUWASA, Wizara ya Ardhi na Viongozi wa Serikali za Mitaa wa maeneo husika.

Katika Eneo la Nzuguni, Wananchi 24 wamelipwa fidia ya Shilingi Milioni 148 ,, Zuzu Nala Wananchi 51 ambao wamelipwa fidia ya Shilingi Milioni 594 ,Nala Chihoni Wananchi 7 ambao walilipwa fidia yao ya Shilingi Milioni 58 na Kanda ya Kibaigwa Wananchi 23 wamelipwa fidia ya Shilingi Milioni 197 na kukamilisha zoezi hilo.

Akizungumzia hatua hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutoa kiasi hicho cha fedha kwa wananchi waliyotoa ardhi yao kupisha utekelezaji wa miradi ya maji.