Dodoma FM

Yafahamu maua kwa ishara ya usafi na uwiano wa asili

14 August 2025, 5:40 pm

Picha ni Bustani ya maua iliyo tengenezwa vizuri kwaajili ya kupendezesha mazingira.Picha na Google.

Ethaning Flowers wanaamini kuwa utunzaji wa mazingira na maua ni mambo yanayoshirikiana kwa karibu.

Na Lilian Leopold.

Katika ulimwengu wa leo unaokabiliwa na changamoto za mabadiliko ya tabianchi na uchafuzi wa mazingira, Ethaning Flowers wamejipambanua kama taasisi inayothamini uzuri na uhai wa mazingira. Kwao, maua si mapambo tu  bali ni ishara ya usafi, afya, na uwiano wa asili.

Ethaning Flowers wanaamini kuwa utunzaji wa mazingira na maua ni mambo yanayoshirikiana kwa karibu. Wanasema, unapolinda udongo dhidi ya mmomonyoko, unapopanda mimea rafiki wa mazingira, na unapohakikisha hakuna taka zinazochafua, unakuwa umeandaa mazingira bora kwa maua kukua kwa afya na rangi ang’avu.

 Vilevile, maua yanapokua, yanasaidia kurudisha uhai kwenye mazingira kwa kutoa hewa safi, kuwalisha nyuki na vipepeo, na kupunguza joto katika maeneo yenye majengo mengi.

Ethaning Flowers wamekuwa mfano wa jinsi biashara inaweza kushirikiana na asili. Kwa kuhamasisha watu kupanda maua na kutunza bustani zao kwa njia rafiki kwa mazingira, kama anavyoelezea Bi. Suzan Kabogo.

Sauti Ethening.