Dodoma FM
Dodoma FM
12 August 2025, 1:30 pm

Picha ni Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD), Mhe. Mwajuma Noty Mirambo wakati akichukua fomu hapo jana Hafla hiyo imefanyika kwenye ofisi za Tume zilizopo Njedengwa Jijini Dodoma.Picha na Tume ya uchaguzi.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii wamesema ni muda muafaka kwa wananchi kutambua sera na Vipaumbele vya wagombea na vyama vyao.
Na Seleman Kodima.
Baada ya kuanza kwa Zoezi la Uchukuaji Fomu za Urais ambapo Vyama vya Siasa kupitia Wagombea wake wamejitokeza kuchukua fomu hizo, Wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii wamesema ni muda muafaka kwa wananchi kutambua sera na Vipaumbele vya wagombea na vyama vyao.
Akizungumza kwa Njia ya Simu Mchambuzi wa Masuala ya Kisiasa kutoka Jijini Dodoma Ismaili amesema zoezi hilo linabeba taswira ya uwepo wa demokrasia katika taifa.