Dodoma FM
Dodoma FM
7 August 2025, 2:21 pm

Watanzania wanaweza kunufaika na udhamini wa mikopo hiyo kwa kupokea huduma za fedha kupitia taasisi zilisajiliwa na kusimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania.
Na Lilian Leopold.
Serikali katika kuhakikisha inaweka mazingira rafiki kwa wajasiriamali imeanzisha mfuko wa udhamini wa mikopo kwa ajili ya kuwawezesha na kuhakikisha wajasiriamali wa wadogo na wa kati kwa wanapata mitaji, mfuko huo ulianzishwa mwaka 2005-2006 .
Akizungumza katika maadhimisho ya Sikukuu ya Nane nane Mchambuzi wa masuala ya fedha, Ezekiel Mwaituka Michael amesema lengo la mfuko huo ni kuhakikisha wajasiriamali wanapata mtaji ili kuendeleza kazi zao.

Kwa upande wake, Ladislaus Sarapioni ambaye ni Mchumi kutoka Benki Kuu ya Tanzania, Kurugenzi ya Tafiti na Sera za Uchumi amesema Benki kuu ya Tanzani inahakikisha inatoa mikopo ili kukuza sekta ya kilimo kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wakulima.
Watanzania wanaweza kunufaika na udhamini wa mikopo hiyo kwa kupokea huduma za fedha kupitia taasisi zilisajiliwa na kusimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania kupitia sheria ya benki na Taasisi za fedha ya mwaka 2006, ambapo mkulima anatawasilisha ombi lake.