Dodoma FM

Jamii yatakiwa kuzingatia suala la unyonyeshaji

6 August 2025, 1:12 pm

Takwimu za hivi karibuni za Tanzania Demographic and Health Survey (TDHS-MIS 2022) zinaonyesha kuwa asilimia kubwa ya watoto wananyonyeshwa angalau mara moja katika maisha yao.Picha na UNICEF.

Wizara ya Afya inaendelea kuhimiza utekelezaji wa sera na hatua za kuimarisha mazingira yanayowawezesha mama kunyonyesha kwa uhuru.

Na Lilian Leopold.
Jamii imeshauriwa kuzingatia suala ya unyonyeshaji kwa watoto ikiwa ni njia ya ustawi wenye afya bora kwa watoto.

Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji kwa Wakina Mama ni kipindi maalum ambacho huadhimishwa kila mwaka kuanzia Agosti 1 hadi 7 duniani kote, Lengo kuu la wiki hii ni kuhamasisha, kulinda na kuendeleza unyonyeshaji wa maziwa ya mama kama njia bora ya kuwapatia watoto lishe kamili, afya bora na kuimarisha uhusiano wa mama na mtoto.

Akizungumza na wakina mama wajawazito na wenye watoto wachanga katika Kituo cha Afya Ilazo, Afisa Lishe jiji la Dodoma, Alpha Fanuel amewaasa wakina mama kuzingatia unyonyeshaji kwa lengo la kumlinda mtoto ili akue kiakili na kimwili.

Sauti ya Afisa Lishe.

Katika kuadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji, baadhi ya wakina mama na wakina baba waliopata elimu kuhusu unyonyeshaji wamekuwa mstari wa mbele kueleza umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto na kwa mama mwenyewe.

Sauti ya baadhi ya akina mama
Juhudi za kuongeza kiwango cha unyonyeshaji wa pekee bado zinaendelea kutekelezwa.Picha na UNICEF.

Takwimu za hivi karibuni za Tanzania Demographic and Health Survey (TDHS-MIS 2022) zinaonyesha kuwa asilimia kubwa ya watoto wananyonyeshwa angalau mara moja katika maisha yao, huku juhudi za kuongeza kiwango cha unyonyeshaji wa pekee zikiendelea kutekelezwa.

Hata hivyo, Wizara ya Afya inaendelea kuhimiza utekelezaji wa sera na hatua za kuimarisha mazingira yanayowawezesha mama kunyonyesha kwa uhuru, ikiwemo likizo ya uzazi, vyumba maalum kazini, na elimu kwa familia nzima. Huku kauli mbiu ya Wiki ya Unyonyeshaji: “Thamini unyonyeshaji: Weka mazingira wezeshi kwa mama na mtoto”.