Dodoma FM

Serikali yatilia mkazo haki na usawa kwa wanawake

6 August 2025, 9:49 am

Picha ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano la Tathmini ya Utekelezaji wa Programu ya Kizazi chenye Usawa.Picha na Maendeleo ya jamii.

Ikumbukwe kwamba Programu ya Kizazi Chenye Usawa Tanzania (Tanzania Generation Equality Program). Utekelezaji wake unahusisha Wadau wa Sekta za Umma na Binafsi katika kipindi cha Miaka Mitano (2021/22 -2025/26).

Na Mariam Matundu.
Waratibu wa Programu ya kizazi chenye usawa (GEF) ngazi ya Halmashauri na Mikoa wametakiwa kutoa taarifa kwa jamii kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa programu hiyo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano la Tathmini ya Utekelezaji wa Programu ya Kizazi chenye Usawa Ngazi ya Halmashauri na Mikoa ambapo washiriki wanajadiliana kuhusu mafanikio, changamoto zilizopo katika utelekelezaji wa programu ya kizazi chenye usawa ya miaka mitano iliyoanza mwaka 2021/2022 hadi 2025/2025.

Aidha, amewaagiza waratibu hao kuwasilisha taarifa za robo mwaka za utekelezaji wa Programu kwa Wizara yenye dhamana ya uratibu kwa wakati ili kusaidia uandaaji wa taarifa ya nchi ya utekelezaji wa Programu ya miaka 5 na kuendelea kutumia na kuzitangaza fursa zilizopo katika maeneo yao, zitakazosaidia utekelezaji bora wa Programu.

Sauti ya Mh. Dorothy Gwajima.
Picha ni Waratibu wa Programu ya kizazi chenye usawa (GEF) ngazi ya Halmashauri na Mikoa wakiwa katika picha ya pamoja na wageni walio hudhuria kongamano hilo.Picha na Maendeleo ya jamii.

Amesema maeneo mengine ni Upatikanaji na umiliki wa rasilimali za uzalishaji kwa wanawake na na kubuni na kutekeleza mipango ya uchumi mkuu inayozingatia jinsia, maboresho ya bajeti na motisha ili kupunguza idadi ya wanawake na wasichana wanaoishi katika umasikini.

Akitoa salamu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto – Zanzibar, Katibu mkuu wa wizara hiyo, Abeida Rashid amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi inashukuru kwa mwaliko wa kushiriki Kongamano hili ambalo kwa upande wetu ni fursa ya kujifunza na mambo mbalimbali yaliyoweza kufanikisha matokeo chanya ya utelekezaji wa programu.