Dodoma FM
Dodoma FM
22 July 2025, 12:20 pm

Mkoa wa Dodoma una idadi kubwa ya vijana wenye umri wa miaka 15–35, ambao ni sehemu muhimu ya nguvu kazi ya taifa ambapo Asilimia 81 ya waliotoa maoni kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 walikuwa vijana wa umri huo.
Na Victor Chigwada.
Ili kukabiliana na changamoto ya Ajira ,Wanafunzi wanaohitimu vyuo vya kati wameiomba Serikali kuwasaidia mitaji ili wanapomaliza masomo yao kutumia taaluma zao kujiingizia kipato.
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya 2022, vijana ni asilimia 34.5 ya Watanzania wote ambapo Vijana wanne 4 kati 10 hawana ajira au fursa za kujikwamua kiuchumi.
Aidha Umoja wa Vijana Wasio na Ajira Tanzania (UYAM) umeeleza kuwa ukosefu wa ajira umepelekea baadhi ya vijana kujiingiza kwenye ubashiri wa michezo na hata kuuza miili yao kama njia ya kujipatia kipato.
Baadhi ya Vijana wakizungumza na Taswira ya habari wamesema kuwa pamoja na jitihada za uwezeshaji wa fani mbalimbali lakini bado changamoto ni mitaji ya kupata vifaa vya kuendeleza fani hizo.
Ng’washi Muhuri ni afisa Serikali inapaswa kuangalia namna ya kuweka mikakati ya kijana mmoja kuweza kunufaika ni mikopo inayotolewa na halmashauri ili kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.