Dodoma FM
Dodoma FM
18 July 2025, 5:07 pm

Malalamiko 11 tayari yamefanyiwa kazi kwa hatua ya awali ya kuwahoji watuhumiwa, huku uchambuzi wa kina ukiendelea.
Na Kitana Hamis.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Kilimanjaro imewahoji watia nia 11 wa ubunge kutokana na malalamiko ya rushwa yaliyowasilishwa dhidi yao, ikiwa ni sehemu ya hatua za mapema za kuchuja wagombea wasio waaminifu kabla ya uteuzi rasmi wa wagombea kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Akizungumza katika semina maalum ya mapambano dhidi ya rushwa iliyoandaliwa kwa watia nia wa ubunge wa mjimbo ya Moshi mjini,Vunjo na Moshi vijijini Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoa wa Kilimanjaro , Mussa Chaulo, alithibitisha kuwa taasisi hiyo imepokea malalamiko mbalimbali na tayari imeanza kuyachakata ili kubaini ukweli wake.
Amesema malalamiko 11 tayari yamefanyiwa kazi kwa hatua ya awali ya kuwahoji watuhumiwa, huku uchambuzi wa kina ukiendelea ili kuhakikisha hakuna mtu anayechafua uongozi wa umma kwa kutumia fedha au ushawishi haramu.