Dodoma FM

Wadau wahimizwa usimamizi usalama wa mabwawa

17 July 2025, 3:50 pm

Picha ni Mkurugenzi ufuatiliaji na tathmini kutoka Wizara ya maji Dkt Diana Kimario akiongea na waandishi wa habari kuelekea kwenye Mkutano wa mwaka wa usalama wa Mabwawa.Picha na Farashuu Abdallah.

Kwa upande mwingine Wataalamu na Wamiliki wa Mabwawa ya maji na tope sumu, Taasisi na watu binafsi wameshauriwa kujisajili katika mafunzo haya muhimu yanayohusu Tahadhari za dharura za kukabiliana na Majanga ya Mabwawa ya Maji na Tope Sumu.

Na Farashuu Abdallah.

Wadau wamehimizwa kusimamia ulinzi wa mazingira hususani maji chini ya ardhi na usalama wa mabwawa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi ufuatiliaji na tathmini kutoka Wizara ya maji Dkt Diana Kimario katika maandalizi kuelekea kwenye Mkutano wa mwaka wa usalama wa Mabwawa ulioandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Chemba ya Migodi Tanzania na kampuni ya City Engineering utakaofanyika jijini Mwanza tarehe 19 hadi 21 Novemba 2025.

Dkt Kimario amesema jukumu la kusimamia  Mabwawa ya maji na tope sumu migodini  siyo tu  la Wizara ya Maji bali ni la Wadau wote pamoja na Wananchi.

Kwa upande wake Dkt George Lugomela Mkurugenzi wa Rasilimali za maji amesema Mkutano huu wa usalama wa Mabwawa utakuwa na tija kwa jamii kwani utatoa Elimu kwa  Wananchi ya namna ya kuchukua tahadhari kwa wale waliokaribu na mabwawa endapo mabwawa hayo yatapasuka.

Naye Mtendaji wa Chemba ya Madini Dkt Benjamini Mchwampaka amemshukuru Mkurugenzi ufuatiliaji na tathmini kwa kuzindua Mkutano wa mwaka wa usalama wa Mabwawa kwani utasaidia kuleta Washiriki wengi zaidi katika kuhakikisha usalama wa Mabwawa unazidi kuimarika.

Habari kamili.