Dodoma FM
Dodoma FM
16 July 2025, 3:17 pm

Hata hivyo ikumbukwe kuwa askari wa kike ni mama kama mama wengine na wanafanya majukumu yao ya kila siku ya kuhudumia familia na watoto ukiachilia mbali na majukumu yake ya kazi.
Na Lilian Leopord.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gallus Hyera amesema uwepo wa askari wanawake imekuwa tija kwa taifa kwani wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha amani, ulinzi na usalama unakuwepo.
Kauli hiyo ameitoa jijini Dodoma wakati akifungua hafla ya mafunzo polisi mtandao wanawake yaliyo wakutanisha askari wanawake Mkoa wa Dodoma ambapo amesema jeshi linatamani askari wa kike wawe mstari wa mbele kufanikisha zoezi la ukamati wahalifu wa kike.

Kamishana Msaidizi wa Polisi ambaye ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Mkoa wa Dodoma Eva Michael ameelezea lengo la semina hiyo ni kuwakutanisha pamoja askari wa kike na kuiondolea jamii dhana potofu iliyo jengeka kwao .
Nao washiriki wa semina hiyo wamesema wameelezea jinsi walivyonufaika na mafunzo hayo.