Dodoma FM
Dodoma FM
9 July 2025, 3:50 pm

Dodoma Tv imezungumza na baadhi ya Wanafunzi ili kujua sababu inayopelekea mabadiliko ya tabia.
Na Farashuu Abdalla.
Imeelezwa kuwa mabadiliko ya tabia kwa baadhi ya Wanafunzi wa Elimu ya juu pindi wanapoingia vyuoni imekuwa ni huzuni na janga katika jamii.
Dodoma Tv imezungumza na baadhi ya Wanafunzi ili kujua sababu inayopelekea mabadiliko ya tabia pindi wawapo vyuoni.
Kwa upande wake Mwanasaikolojia na Mbobezi wa Malezi Mtahu Mtahu amesema sababu ya mabadiliko ni tamaa kwa baadhi ya Wanafunzi huku akimaliza kwa kutoa ushauri kwa Wanafunzi na jamii kiujumla.