Dodoma FM
Dodoma FM
2 July 2025, 10:21 am

Jitihada za kumwokoa hazikufanikiwa.
Na Kitana Hamis.
Kijana mmoja aitwaye Fredy Peter, mkazi wa Kijiji cha Seleto, Dareda Misheni, Wilaya ya Babati mkoani Manyara, amefariki dunia baada ya kushambuliwa na kundi la fisi .
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, walisikia sauti zisizo za kawaida usiku huo na walipoamua kufuatilia, walikuta kundi la fisi likimvamia mtu na awali walidhani ni mnyama wa kawaida kama ndama. Hata hivyo, walipokaribia walibaini kuwa aliyekuwa akishambuliwa ni binadamu.
Jitihada za kumwokoa hazikufanikiwa kutokana na ukali wa shambulio hilo, ambapo kijana huyo alifariki dunia katika tukio hilo la kusikitisha.
Wananchi wameiomba Serikali na mamlaka za wanyamapori kuchukua hatua za haraka kudhibiti wanyama wakali wanaovamia makazi ya watu na kuhatarisha maisha .