Dodoma FM
Dodoma FM
27 June 2025, 10:11 am

Ni muhimu kutambua kundi la watu wenye ulemavu wa uziwikutoona.
Na Mariam Kasawa.
Imeelezwa kuwa licha ya Tanzania, kama zilivyo nchi nyingine duniani, kuwa na kundi la Watu wenye Ulemavu ambalo, licha ya kuwa kundi dogo kwa idadi ya watu wote, bado lina umuhimu mkubwa katika maendeleo ya jamii.
Hayo yamesemwa na Kaimu katibu mkuu na naibu katibu mkuu ofisi ya waziri mkuu kazi vijana ajira na watu wenye ulemavu Bi. Zuhura Yunus katika uzinduzi wa kitovu cha kimataifa cha rasilimali za uziwikutoona uliofanyika leo jijini Dodoma.

Amesema ni muhimu kutambua kundi la watu wenye ulemavu wa uziwikutoona (deafblindness) kama sehemu dogo ya ndani ya kundi hili na mara nyingi kundi hili halionekani kwenye takwimu rasmi
Rutachwamagyo Kaganzi ni mjumbe wa bodi kutoka Sense Internatinal Tanzania anasema uzinduzi wa kitovu cha rasilimali za uziwikutoona itasaidia sana jamii kwani viziwiwa kutoona ni watu wanao hitaji kufahamu vitu vingi kwa kupata maarifa.

Nae Mwalimu Maura Ulaya mkuu wa kitengo cha viziwiwasioona kitengo cha uhuru mchanganyiko anasema kwasasa teknolojia inasaidia sana katika ufundishaji wa wanafunzi hawa ambapo hapo awali ilikuwa ngumu kwao kujifunza kwa urahisi.