Dodoma FM
Dodoma FM
25 June 2025, 3:46 pm

Mwezi juni kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya kupiga vita dawa za kulevya ambapo maadhimisho hayo hufanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzia june 24 ,25 na 26
Na Anwary Shaban.
Katika kuadhimisha siku ya kupiga vita dawa za kulevya duniani wananchi mkoani Dodoma wamehimizwa kupata elimu ya athari za matumizi ya dawa hizo.
Wito huo umetolewa na mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule wakati akizungumza na wananchi katika ukumbi wa Jakaya kikwete jijini Dodoma yanapo fanyika maadhimisho hayo.
Mh.Senyamule amesema dawa za kulevya ni janga linalo athiri familia nyingi nchini ,hivyo ni muhimu kwa wananchi kushiri kikatika maonesho hayo.

Aidha Mh.Senyamule amebainisha lengo la maadhimisho hayo kuwa ni kupaza sauti kwa umma juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya.
Mwezi juni kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya kupiga vita dawa za kulevya ambapo maadhimisho hayo hufanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzia june 24 ,25 na 26 ambapo kilele cha maadhimisho hayo kwa hapa nchini kinatarajiwa kufanyika jijini Dodoma huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.