Dodoma FM
Dodoma FM
18 June 2025, 1:25 pm

Simulizi yetu inatupeleka katika kijiji cha Chali Igongo, wilayani Bahi mkoani Dodoma
Katika maeneo mengi ya vijijini nchini Tanzania, mabadiliko ya tabia nchi yamekuwa tishio la kweli si kwa mazao tu, bali kwa maisha ya kila siku ya wanawake na watoto.
Ukame umegeuka kuwa mgeni wa kudumu. Vyanzo vya maji vinaendelea kukauka. Wanawake wanalazimika kutembea zaidi ya kilomita tano kusaka tone la maji jukumu ambalo kwa miongo mingi limeonekana kuwa la kawaida, lakini sasa limejaa hatari.
Hatari ya kubakwa, kupigwa, au kutukanwa njiani wakati wa kutafuta maji ni changamoto inayowakumba wanawake wengi. Ukatili huu wa kijinsia unaochochewa na mazingira siyo tu kwamba unafichwa, bali pia haujatambuliwa kwa kina katika sera na mikakati ya kitaifa.

Msikilizaji leo katika Makala yetu tunaangazia suala la mabadiliko. Katika sura ya ukame na uhaba wa maji ambao unachochea kwa kiasi kikubwa katika kuchangia vitendo vya ukatili hasa katika sehemu za vijijini.
Katika makala hii, tutasikia simulizi za wanawake waliokumbwa na madhila hayo, tutazungumza na viongozi wa kijiji, wataalamu wa kijinsia, pamoja na wanaharakati wanaopigania haki za wanawake vijijini.
