Dodoma FM
Dodoma FM
10 June 2025, 3:55 pm

Wakazi hao wameishukuru Serikali kwa kukamilisha hospitali hiyo ya Wilaya kwani imewapunguzia gharama za kusafiri kwenda hospitali zingine.
Na Victor Chigwada.
Ujenzi wa hospitali mpya ya Wilaya ya Chamwino katika Kata ya Mlowa barabarani umetajwa kuongeza tija kwa wananchi na kuwapunguza changamoto za kusafiri umbali mrefu kufuata huduma.
Wakazi wa Mlowa Barabarani wanasema hapo awali iliwalazimu kufuata huduma za afya katika hospitali za Mvumi Mission pamoja na hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma hali iliyo hatarisha usalama wa wagonjwa wakiwemo akina mama wajawazito.
Aidha wakazi hao wameishukuru Serikali kwa kukamilisha hospitali hiyo ya Wilaya kwani imewapunguzia gharama za kusafiri kwenda hospitali zingine
Diwani wa Mlowa barabarani Anjero Lucas amekiri hospitali hiyo kuleta tija Kwa wakazi wa Mlowa na maeneo jirani kwani imeendelea kuboreshwa nakutoa huduma ambazo awali hazikuwepo.